- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis, ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupanda miti kwa wingi na kuitunza kwa uangalifu ili kukabiliana na changamoto za jangwa na ukame zinazoikumba nchi.
Mhe. Khamis ameyasema haya leo, Juni 17, 2025, katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame, ambayo kitaifa yamefanyika katika Manispaa ya Shinyanga ambapo amesisitiza kuwa kupanda miti na kutunza mazingira ni hatua muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
“Maadhimisho haya yanatukumbusha wajibu wetu wa kulinda mazingira dhidi ya jangwa na ukame. Tuendelee kupanda miti ya kutosha, lakini pia tuhakikishe kuwa shughuli za kilimo na ufugaji zinafanyika kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira. Lengo letu ni kuilinda ardhi yetu, tuungane kuiokoa Tanzania,” amesema Mhe. Khamis.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Wakili Julius Mtatiro, ameeleza kuwa wilaya ya shinyanga imeweka mikakati ya kulinda miti iliyopandwa kwa kuimarisha utekelezaji wa sheria ndogo dhidi ya ukataji miti holela kwa kuweka sheria ndogo pamoja na adhabu kwa wale wanaokata miti kiholela, huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kuitunza miti tuliyopanda kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Naye Mkuu wa Idara ya Maliasili na Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Ezra Manjerenga, amebainisha kuwa matumizi ya kuni kwa wingi katika kupikia yamewahi kusababisha madhara kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na athari za kiafya,hali iliyosababisha mauwaji ja vikongwe kutokana na Imani za kishirikina hali iliyosababishwa na matumizi ya kuni.
Maadhimisho ya siku ya umoja wa mataifa ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa duniani kitaifa yanmefanika Halmashauri ya manispaa ya shinyanga yakiongozwa na kaulimbiu isemayo: “ONGOA ARDHI KUFUNGUA FURSA”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga