- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
TENGENEZENI TIMU MAALUM YA KUSHUGHULIKIA HOJA ZA CAG - RC MACHA
Na. SHINYANGA MC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amezielekeza Halmashauri zote 6 zinazounda Mkoa kutengeneza timu maalum kwa ajili ya kushughulikia hoja mbalimbali za Mdhibiti na Mkuguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na nyinginezo kwa lengo la kuziondoa kuzipunguza kama siyo kuzifuta kabisa huku akisisitiza kuongezwa juhudi za ukusanyaji mapato na utoaji wa elimu ya wananchi kuwa na uhiari wa kulipa bila shuruti ili miradi ya Serikali iweze kutekelezeka.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 25 Juni, 2024 alipokuwa akitoa mchango wake katika Baraza Maalum la kujadili mapendekezo ya hoja za CAG katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na kuwapongeza kwa kupata Hati Safi ya CAG lakini pia wameibuka washindi namba 1 katika mashindano ya Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji katika Usafi wa Mji na Utunzaji wa Mazingira pamoja na kushika nafasi ya 18 Kitaifa katika utoaji wa habari dhidi ya Halmashauri 184 ushindi ambao unaiongezea morali Manispaa katika utendaji kazi wake.
“Nizielekeze sasa Halmashauri zote ndani ya Mkoa kuangalia namna ya kutengeneza Timu Maalum isiyozidi watu watano itakayokuwa na jukumu la kushughulikia hoja za CAG wakati wote badala ya kusubiria wakati wa ukaguzi ndiyo wataalam waanze kupambana na hoja hizi, kwa kufanya hivi Halmashauri zitapunguza kama siyo kuzimaliza kabisa na kuendelea kupata Hati Safi,” amesema RC Macha.
Pamoja na mambo mengine Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo amezishauri Halmashauri kuachana na mpango wa kuanzisba miradi mipya, badala yake ishughulike na umaliziaji wa vipolo vya miradi ya mwaka uliopita huku akisisitiza kuwa ni vema mradi unapoanzishwa utekelezwe mpaka mwisho kisha ndiyo uanzishwe mwingine, kwa kufanya hivi tija ya miradi itaonekana.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amesema, Manispaa ilikuwa na hoja 43 ambapo 7 zimefungwa na 36 hazijafungwa huku ikitekeleza maagizo manne ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na kubaki na agizo 1 ambalo lipo katika hatua za utekelezaji.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga