- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze Leo Disemba 5 , 2024 amefanya ziara ya kishtukiza ya kutembelea miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya shinyanga.
Mwl. Kagunze ameweza kufanya ziara ya kushtukiza katika ujenzi wa shule mpya ya sekondari iliyopo kata ya Kizumbi, ujenzi wa nyumba za walimu shule ya sekondari butengwa kata ya ndembezi pamoja na ujenzi wa mabweni manne shule ya sekondari rajani kata ya kolandoto manispaa ya shinyanga na kuonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na kuwataka wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa miradi kujenga kwa haraka ili kukamilisha kwa wakati na kwakuzingatia ubora wa ujenzi.
“Siridhishwi kabisa na kasi hii ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika shule hii mpya, serikali imeleta fedha nyingi ili kutekeleza miradi hii lakini utekelezaji unakua hafifu, hatuwezi tukamvumilia mkandarasi mvivu anae chelewesha miradi ya serikali kukamilika , Kama mtaendelea na kasi hii ndogo tutasitisha mikataba yenu ili tuwapatie wakandarasi wanao weza kutekeleza miradi ndani ya muda elekezi ili wanafunzi waweze kusoma vizuri kwa nafasi”. Amesema MD Kagunze.
Katika hatua nyingine Mwl. kagunze ametumia fursa hiyo kuwaagiza walimu wote wa shule za msingi na sekondari kupanda miti pamoja na kuitunza miti ya matunda na vivuli katika maeneo yote ya shule ili kutunza mazingira katika msimu huu wa mvua.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga