- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa, amesema kuwa Serikali imejipanga kuendelea kuiboresha Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga (Shinyanga Girls Secondary School), ili kuiwezesha kuwa miongoni mwa Shule bora zaidi nchini Tanzania.
Ndg. Msigwa alitoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya kikazi mkoani Shinyanga, akiwa ameambatana na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Shinyanga na Mwanza, kwa lengo la kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akiwa katika shule hiyo, Ndg. Msigwa ameeleza kuwa Serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 4 katika ujenzi wa miundombinu ya Shule hiyo ili kutoa mazingira rafiki kwa wanafunzi wa kike kujifunza na walimu kufundisha kwa ufanisi, ambapo amesema juhudi za maboresho zaidi zitaendelea ili kuifanya shule hiyo kuwa ya mfano kitaifa.
“Shule ya Wasichana Shinyanga ni mradi wa kimkakati katika kuwekeza kwa wasichana kielimu. Serikali itaendelea kuboresha mazingira haya ili kuifanya shule hii kuwa miongoni mwa shule bora kabisa nchini,” amesema Ndg. Msigwa.
Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga ni mojawapo ya shule 26 maalum za wasichana nchini, ambapo ilianza rasmi kupokea wanafunzi mwaka 2023 kwa ngazi ya kidato cha kwanza na cha pili, pamoja na kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita kwa mchepuo wa Sayansi.
Katika ziara hiyo, Ndg. Msigwa pia ametembelea uwanja wa ndege wa Shinyanga uliopo katika Kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga, unao gharimu jumla ya bilioni 44.8 ambapo ameeleza kuwa ujenzi wake umefikia asilimia 80 ya utekelezaji ambapo inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2025
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga