• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Fedha
      • Ujenzi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Hearth
      • Usafi na Mazingira
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Tecknolojia, Habari, Mawasiliano na Uhusiano
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Nyuki na Maliasili
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uwekezaji wa Viwanda
    • Fursa za kilimo
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Fursa za elimu
    • Fursa za Afya
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma ya utoaji wa Mikopo
    • Kukondisha Vyumba vya Biashara
    • Unyonyaji wa Maji Taka
    • Huduma za Biashara
      • Leseni za Biashara
      • Elimu ya kibiashara
      • Ukaguzi wa Viwanda
      • Usimamizi wa Masoko
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Miundombinu
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya kamati za Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iIliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Mafunzo

RC SOPHIA MJEMA AZINDUA RASMI KAMPENI YA UPANDAJI MITI YA 'PENDEZESHA TANZANIA'

Posted on: December 4th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  amezindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB inayolenga kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumamosi Desemba 4,2021 katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara na Madini wa Butulwa maarufu viwanja vya Zainab Telack uliopo kata ya Old Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga ambapo pia wananchi wamepatiwa miti bure kwa ajili ya kwenda kupanda kwenye maeneo yao.

Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuja na Programu ya Pendezesha Tanzania kwa kuhamasisha upandaji wa miti na utunzaji mazingira nchini kupitia kanda zake 7 za Kibenki.

“Kwa upande wa Kanda ya Magharibi mkoa wetu wa Shinyanga umebahatika kuwa chaguo la Benki ya CRDB kuendesha Programu hii kupitia kwenye viwanja vyetu vya maonesho ya Biashara na Madini vya Zainab Telack. Hadi leo katika viwanja hivi Benki ya CRDB wamekwisha panda takribani miti 1,000 na leo imekusudiwa kupandwa miti 900 ili kufikisha adhima yao ya kupanda miti 2,000. Naomba tuwapongeze”,amesema Mhe. Mjema.

“Napenda kuwashukuru Benki ya CRDB kwa kuendesha Programu hii ya Kizalendo . Pia nawashukuru wadau wote mliojitokeza katika zoezi hili la upandaji miti. Napenda kuzihamasisha taasisi zote zilizopo mkoani Shinyanga kwa kuiga na kuunga mkono juhudi hizi ambazo wenzetu Benki ya CRDB wamezionesha kwa Programu yao ya PendezeshaTanzania kwa kupanda miti na kuhamasisha utunzaji mazingira”,ameongeza Mjema.

Mkuu huyo wa mkoa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za utunzaji mazingira na uwekaji wa mikakati ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi zilizopelekea kupata fedha za Mfuko wa Utunzaji Mazingira (GCF).

Mjema amesema Mkoa wa Shinyanga umejipanga kupanda miti Milioni 9 na sasa miti milioni 5 imepatikana tayari kwa kuanza kupandwa huku akiagiza Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanasimamia upandaji miti na miti iliyopandwa.

Amefafanua kuwa dunia kwa ujumla inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi yanayochangiwa shughuli za kibinadamu hususani ukataji miti na ukuaji wa viwanda ambao unasababisha ongezeko la gesi ukaa hali inayosababisha ukosefu wa mvua za kutosha na zisizotabilika na ongezeko la joto na kuyeyuka kwa barafu katika Mlima Kilimanjaro.


“Kwa ujumla hali siyo nzuri, sisi sote ni mashahidi siku hizi hata msimu wa mvua haueleweki hivyo kusababisha mavuno hafifu, ukosefu wa maji ya uhakika. Mwarobaini wa haya ni sisi kuamua kwa dhati kutunza mazingira hasa kwenye vyanzo vya maji kwa kupanda miti na kuachana na ukataji miti ovyo kwa faida yetu pamoja na vizazi vijavyo”
,ameeleza.

“Wananchi wa Shinyanga tuhakikishe katika makazi yetu tunatunza mazingira na kupanda miti hususani miti ya matunda,vivuli na mbao ili kuifanya dunia iwe sehemu salama ya kuishi”,amesema.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amesema tayari wilaya ya Shinyanga inaendelea na Kampeni ya Upandaji miti ya ‘Shinyanga ya Mikwaju na Miembe’ hivyo kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika upandaji miti na utunzaji mazingira.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndugu Jomaary Satura Akishiriki kikamilifu Zoezi hilo na Kuacha Alama ya Upandaji wa Mti aina ya Muembe

Wanafunzi kutoka Shule Mbalimbali Ndani ya Manispaa Walishiriki Kampeni hiyo

Meya wa Manispaa Ya Shinyanga Mh Elias Ramadhani Masumbuko Akishiriki kwenye Kampeni hiyo




Wadau Mbalimbali Walijitokeza Kuiunga Mkono Serikali kwa Kampeni ya Kupanda Miti ya Pendezesha Tanzania

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • Tazama

Habari Mpya

  • ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    May 08, 2025
  • MHE.MASUMBUKO AWATAKA MADIWANI KUSHIRIKIANA KIKAMILIFU KUKABILIANA NA WIZI WA VIFAA VYA MIRADI YA MAENDELEO.

    May 07, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MAAGIZO

    May 06, 2025
  • SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA SHULE YA WASICHANA SHINYANGA ILI KUIFANYA KUWA MIONGONI MWA SHULE BORA NCHINI “. NDG. MSIGWA.

    May 03, 2025
  • Tazama

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
Video Zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Ripoti mbalimbali
  • Sheria Ndogondogo za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Tovuti Nyingine tunazohusiana

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa(TAMISEM)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknologia
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Mkoa wa Shinyanga
  • Sekretarieti ya Ajira

wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Tanesco S, Mwanza Road

    Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga

    Simu: +255-28-2763213

    Simu ya Mkononi: 0759 023 788

    Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Ramani ya Tovuti
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga