• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Fedha
      • Ujenzi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Hearth
      • Usafi na Mazingira
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Tecknolojia, Habari, Mawasiliano na Uhusiano
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Nyuki na Maliasili
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uwekezaji wa Viwanda
    • Fursa za kilimo
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Fursa za elimu
    • Fursa za Afya
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma ya utoaji wa Mikopo
    • Kukondisha Vyumba vya Biashara
    • Unyonyaji wa Maji Taka
    • Huduma za Biashara
      • Leseni za Biashara
      • Elimu ya kibiashara
      • Ukaguzi wa Viwanda
      • Usimamizi wa Masoko
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Miundombinu
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya kamati za Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iIliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Mafunzo

RC MNDEME AWATAKA WAZAZI NA WALEZI HALMSHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA KUWAPELEKA WATOTO SHULE

Posted on: January 8th, 2024

RC MNDEME AWATAKA WAZAZI NA WALEZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA KUWAPELEKA WATOTO SHULENI


Na. Shinyanga Mc


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amewataka wazazi na walezi wote wa Halmashauri ya Manispaa ya shinyanga kuhakikisha wanawaleta watoto wao wote ambao wanastahili kusoma kwakuwa hakuna tena ada, kila mtoto anayestahili kusoma atapokelewa na hakuna hata mtoto mmoja atakayebakia nyumbani.


Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 8 Januari, 2024 alipotembelea shule ya Awali na Msingi Mwenge, shule ya Sekondari Ngokolo pamoja na shule ya Sekondari Wasichana Shinyanga zote za Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine pia amewapongeza sana walimu wote wakiongozwa na Maafisa Elimu wao wote kwa kazi nzuri wanazozifanya ikiwàmo kufundisha, kuhamasisha na kuandikisha watoto wapya.


"Nawaomba sana wazazi na walezi wote wenye watoto wanaostahili kusoma muwalete shuleni, hakuna atakayewadai ada,na hasa wenye ulemavu msiwafiche na kuwaacha nyumbani waleteni shuleni kila kitu ni bure", amesema Mhe. Mndeme.


Pamoja na mambo mengine Mhe. Mndeme amewaeleza wanahabari na walimu waliokuwa katika majumuisho ya ziara hii kuwa, Serikali ya mkoa wa shinyanga imefanikiwa kumuokoa mwanafunzi wa kidato cha kwanza 2024 (jina limehifadhiwa) aliyekuwa ameozeshwa na mzazi wake ajulikanaye kwa jina la Dotto Mjanasa maarufu kama Dullah Mjanasa mkazi wa kijiji cha Iyugi, Kata ya Lyamidati Halmashauri ya Shinyanga ambaye alimuozesha kwa jumla ya ng'ombe 15.


Mtoto huyu ambaye amefaulu vizuri sana, amenusuriwa na serikali baada ya wasamalia wema kutoa taarifa haraka serikali ilichukua hatua ya haraka na kwenda kwenye eneo la tukio na baada ya kumkomboa mzazi huyo alikimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea.


Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mwl. Dafroza Ndalichako amesema kuwa kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya 2022, mkoa ulikuwa na maoteo ya kuandikisha wanafunzi wa Awali 75,079 ambapo mpaka sasa wameandikisha wanafunzi 47,182 na kwa darasa la kwanza lengo ni 69,792 huku walioandikishwa ni 44,332 na kwa kidato cha kwanza ni 38,963.

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • Tazama

Habari Mpya

  • MHE. MWEBEA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 05, 2025
  • MUONEKANO WA JENGO OPD KIPINDI CHA UJENZI NA BAADA YA KUKAMILIKA

    June 03, 2025
  • MUONEKANO WA JENGO LA UTAWALA SHULE YA WASICHANA SHINYANGA KIPINDI CHA UJENZI NA BAADA YA KUMALIZA UJENZI

    June 02, 2025
  • WANAFUNZI KUTOKA SHULE 20 ZA MANISPAA YA SHINYANGA WAKUTANA KUBADILISHANA UJUZI ILI KUBORESHA TAALUMA.

    May 17, 2025
  • Tazama

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
Video Zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Ripoti mbalimbali
  • Sheria Ndogondogo za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Tovuti Nyingine tunazohusiana

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa(TAMISEM)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknologia
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Mkoa wa Shinyanga
  • Sekretarieti ya Ajira

wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Tanesco S, Mwanza Road

    Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga

    Simu: +255-28-2763213

    Simu ya Mkononi: 0759 023 788

    Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Ramani ya Tovuti
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga