- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RC MNDEME ASIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 28 Februari, 2024 amesikiliza na kutatua kero za wananchi wa Manispaa ya Shinyanga katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika katika Soko kuu la Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza Mhe. Mndeme wakati wa kutatua kero hizo za wananchi, amewataka Watumishi wa Serikali wafanye kazi kwa weledi katika kuwahudumia wananchi.
Aidha, akijibu kero ya kutokamilika kwa Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga, ametoa maelekezo kwamba hadi kufikia Mei 30 mwaka huu Soko hilo liwe limeshakamilika kujengwa lote na kuanza kutumika.
Amewataka pia Watumishi wa Idara ya Ardhi kufanya kazi zao kwa weledi na umakini ili kuepusha migogoro ya ardhi, ikiwamo kutogeuza matumizi ya ardhi kinyume na utaratibu.
“Kero zote ambazo mmeziwasilisha hapa zitashughulikiwa kwa utaratibu na kila mtu atapata haki yake.” amesema Mhe. Mndeme
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe.Johari Samizi,akijibu kero ya Mikopo umiza, amewataka wananchi wajiepushe na Taasisi ambazo zinakopesha fedha zisizo na vibali wala kutambulika na BOT, na kwamba watakapopata taarifa za Taasisi isiyo sajiliwa wampatie taarifa.
Mhe. Christina Mndeme ameanza leo ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Manispaa ya shinyanga ambapo kesho tarehe 29 Februari, 2024 ataendelea ya ziara hiyo katika Manispaa ya Kahama.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga