- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka Wakazi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 huku akihamasisha wananchi wote wanawake kwa wanaume wenye sifa kuchukua fomu ili kuwania nafasi za uongozi ngazi ya mtaa, kijiji na kitongoji.
Mhe. Macha ametoa rai hiyo leo Jumanne Oktoba 8,2024 wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga litakaloanza tarehe 11.10. 2024 hadi 20.10.2024 likiongozwa na Kauli mbiu “Serikali za mitaa, sauti ya wananchi, jitokeze kushiriki uchaguzi”.
“Akina mama wamechangamka sana safari hii, tuhakikishe tunapata uongozi wa pamoja hivyo niwaombe wanaume kwa wanawake tujitokeze kugombea nafasi za uongozi kwa sababu uchaguzi utafanyika ukizingatia makundi yote”. amesema Mhe. Macha.
Aidha Mhe. Macha amewasihi wananchi wachague viongozi bora na wanaojulikana watakaowaletea maendeleo badala ya kuchagua viongozi mafisadi wa kuhujumu miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga , Mhe. Elias Masumbuko amewataka wananchi kutumia vizuri muda wa kujiandikisha kila mmoja ajiandikishe kwani suala hilo linafanyika kwa misingi ya haki na amani.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Charles Kafutila amesema Manispaa ya Shinyanga ina kata 17, vijiji 17, vitongoji 84 na mitaa 55 na zoezi la uandikishaji wapiga kura litafanyika katika vituo 199 ambapo lengo la Manispaa ni kuandikisha wapiga kura 120,345.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga