- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewasihi wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza Katika wiki ya maadhimisho ya Sheria ili wajue taratibu, haki zao pamoja na taratibu mbalimbali zinazohusiana na Sheria.
RC Macha ameyasema haya leo Januari 25,2025 wakati akifungua wiki ya Maadhimisho ya Sheria kimkoa yanayofanyika Katika viwanja vya zimamoto Nguzonane Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
“Maadhimisho haya ya Wiki ya Sheria ni muhimu sana kwa wananchi, kwani kuna watu wengi wanashindwa kupata haki zao kutokana na kutokujua sheria, hivyo ni vyema mjitokeze kwa wingi kwenye vibanda na wapate elimu ya sheria, namna ya kufungua mashauri mahakamani, pamoja na kujua kazi za Mawakili,”Amesema Mhe. Macha.
Katika hatua nyingine Mhe.Macha ameipongeza Mahakama kuu kanda ya Shinyanga kwa ufanisi wake katika kusikiliza mashauri kwa wakati na kutoa haki kwa wananchi.
Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Ndg. Frank Mahimbali, ameeleza kuwa katika Wiki ya Sheria, elimu ya sheria itatolewa bure kwa wananchi kupitia vibanda mbalimbali vilivyopo viwanja vya Zimamoto na maeneo ya mikusanyiko, magereza, mashuleni na vyuo.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka huu ni: “Tanzania 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga