- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha,amewasihi Watanzani kuwa enzi mashujaa ambao walipigania taifa hili kupata uhuru,kwa kudumisha amani na upendo.
Mhe. Macha amebainisha hayo leo Julai 25,2024 ikiwa ni siku ya kuwaenzi mashujaa, ambao walilipigania taifa kupata uhuru kwa kutumia silaha za jadi, maadhimisho ambayo katika Mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika mnara wa mashujaa mazingira center Manispaa ya Shinyanga, maadhimisho yaliyojumuisha vikosi vya ulinzi na usalama, watumishi na wananchi mbalimbali na kuweka mashada na silaha za jadi katika mnara.
“Tuwaenzi mashujaa wetu ambao walilipigania taifa hili kupata uhuru, kwa kuendelea kudumisha amani, ya nchi yetu na wale ambao bado wapo hai tuwapongeze na kuwaenzi pia kwa kazi kubwa ambayo waliifanya ya kujitoa kwao ili Tanzania iwe huru,”amesema Mhe. Macha.
“Nawasihi Watanzania tuilinde amani hii ambayo tunayo tusije ichezea, ni heli tufofautiane kwa vitu vingine lakini siyo kuvuruga amani, amani ikitoweka kuirudisha ni kazi,” ameongeza. Mhe Macha
Kila ifikapo Julai 25, ya kila mwaka Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kulinda Uhuru wa Tanzania.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga