- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RC MACHA AONGOZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI NGAZI YA MKOA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na : Shinyanga MC
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Annamringi Macha leo tarehe 1 Mei 2025 ameongoza maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi iliyofanyika kimkoa katika Manispaa ya Shinyanga katika Viwanja vya CCM kambarage sherehe iliyoudhuliwa na viongozi mbalimbali, watumishi kutoka taasisi mbalimbali pamoja na wananchi.
Akizungumza katika maadhimisho haya Mhe. Macha amewata watumishi wote kuendelea kufanya Kazi kwa weledi, ili kuendelea kumuunga mkono juhudi zote anazozifanya Rais wetu Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassani kwa kuboresha mazingira mazuri katika sehemu zetu za kufanyia kazi.
“ Niwatake watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa weledi, sheria na taratibu za kiutumishi ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wetu kwa kuboresha mazingira mazuri katika sehemu zetu za kufanyia kazi “
Amesema Mhe. Macha
katika maadhimisho haya Mhe. Macha awataka pia watumishi wakashiriki katika kupiga kura pamoja na wananchi kwani ni haki yao ya msingi ili wakachague viongozi watakao leta maendeleo, sambamba na kuwata wananchi wote kwa ujumla kushiriki katika zoezi la uboreshaji la daftari la kudumu la kupiga kula awamu ya pili ambapo kwa Manispaa ya Shinyanga zoezi hili limeanza leo tarehe 1-7 Mei 2025 .
Pamoja na mambo mengi Maadhimisho haya yaliambatana na maandamano kutoka viwanja vya zimamoto nguzonane kuelekea uwanja wa CCM Kambarage, michezo mbalimbali kutoka kwa wananchi pamoja watumishi ikiwemo mbio za baiskeli, kuvuta kamba pamoja na nyimbo mbalimbali kutoka kwa wasanii wa kutoka Manispaa ya Shinyanga.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mei Mosi 2025 “ Uchaguzi Mkuu wa 2025 utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote tushiriki:
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga