- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
'RAIS SAMIA NI MSIKIVU ATALIFANYIA KAZI SUALA LA KIKOKOTOO '' RC MACHA
Na. Jesca kipingu SHYMC
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewatoa hofu Watumishi juu ya suala la Kikokotoo, kwamba Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni msikivu na atalifanyia kazi.
Mhe. Macha amebaini hayo Mei 1 , 2024 kwenye Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi dunia (MEIMOSI) ambapo kimkoa wa shinyanga yalifanyika Kata ya Kakola wilayani Kahama alisema suala la Kikokotoo limesemwa vya kutosha kila Mahali hadi Bungeni, na kwamba anaimani Serikali imelisikia na italifanyia kazi kwa Maslahi ya wafanyakazi.
“Tunaye Rais wetu msikivu na atalifanyia kazi suala la Kikokotoo,” alisema Mhe. Macha
Aidha, Mhe. Macha alisema Rais Samia amekuwa akiboresha mara kwa mara Maslahi ya Watumishi wa Umma, pamoja na Mazingira Mazuri ya kufanyia kazi ikiwamo ya nyongeza ya mishahara huku akiwasihi watumishi wa serikali hasa walimu , watumishi wa afya na kilimo kwamba wasijiingize kwenye Mikopo Kausha damu ambayo imekuwa ikiwadumaza Kimaendeleo.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Macha aliwaahidi Watumishi wa Serikali kwamba yale yote ambayo wamewasilisha kwenye Risala yao yanayogusa ngazi ya Kitaifa likiwamo pia suala la Kikokotoo na Vifurishi vya Bima ya Afya atayafikisha sehemu husika tena kwa maandishi.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani Mwaka huu inasema” nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga dhidi ya hali ngumu ya Maisha.”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga