- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na.Shinyanga Mc
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametoa wito kwa Halmashauri zote zinazounda Mkoa wa Shinyanga kuja kujifunza namna ya kuzingatia suala la usafi kutoka kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mhe. Macha ameyasema haya leo septemba 20, 2024 katika maadhimisho ya siku ya usafishaji duniani ambapo kwa mkoa wa Shinyanga maadhimisho haya yamefanyika katika soko la Nguzo Nane lililopo Manispaa ya Shinyanga.
“Ninapendezwa sana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga namna inavyozingatia suala la usafi,halmashauri zote zinazounda mkoa huu wa shinyanga sio dhambi kama mkija kujifunza na kuiga suala la usafi linavyozingatiwa na Manispaa hii ni dhairi hata pongezi mlizopata kutoka Wizarani mnastahili”. amesema Mhe. Macha.
Katika hatua nyingine Mhe. Macha amepiga marufuku kwa mama lishe wote mkoa wa shinyanga wanaohifadhi vyakula vya moto kwenye Mifuko ya plastiki (lailoni) ambavyo vinasababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo kansa.
Maadhimisho haya kidunia yalikuwa yakiongozwa na KAULI MBIU
“UHAI HAUNA MBADALA, ZINGATIA USAFI WA MAZINGIRA “
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga