- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Alexius Kagunze, amewatakia kila la heri wanamichezo wa Manispaa ya Shinyanga wanaokwenda kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA mkoani Tanga, huku akiwasisitiza uwajibikaji, nidhamu na kujituma kwa kila mmoja wao ili kufanikisha ushindi.
Akizungumza leo, Agosti 15, 2025, wakati wa kuagana nao kabla ya kuanza safari, Mwl. Kagunze amesema Halmashauri inaimani kubwa sana na wanamichezo hao kufanya vizuri ili kuhakikisha timu hiyo inapata tuzo.
“Nendeni mkaiwakilishe vyema bendera ya Manispaa ya Shinyanga tunamatumaini kubwa sana na nanyi. Kila mmoja wetu twendeni tukashirikiane, tujitume na kupigania ushindi. Ubora tunao, nia tunayo, na shauku ipo sasa ni wakati wa utekelezaji.” amesema Mwl. Kagunze.
Mashindano ya SHIMISEMITA yameanza Agosti 15 na yanatarajiwa kumalizika Agosti 29, 2025, yakihusisha timu kutoka halmashauri mbalimbali nchini.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga