- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NAIBU WAZIRI MHE. MWINJUMA AZINDUA MASHINDANO YA DKT. SAMIA/KATAMBI MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga MC
Naibu waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma tarehe 14 Julai, 2024 amezindua mashindano ya Dkt, Samia Katambi cup yanayohusisha michezo mbalimbali ikiwemo, Mpira wa miguu, kuimba, kukimbiza kuku, kula, kuvuta kamba, Ngoma za asili, pamoja na mashindano yenye lengo la kuibua vipaji, kuvikuza na kuviendeleza vipaji vilivyomo ndani ya Manispaa ya Shinyanga hususani kwa jimbo la Shinyanga Mjini, mashindano yaliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi.
Akizungumza kwenye ufunguzi huo Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mwinjuma amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo ili kuibua vipaji vyao na kupata ujira kupitia mashindano hayo pamoja na kuboresha afya kupitia mazoezi.
“Niwatake vijana wote kwa ujumla mchangamkie hii fursa ya michezo mbalimbali ili muweze kuibua vipaji mlivyonavyo , kujipatia ajira na kuboresha afya ya mwili kupitia mazoezi” amesema Mhe. Mwinjuma.
Naye Naibu waziri, ofisi ya waziri Mkuu, kazi, vijana, Ajira na wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Patrobas Katambi alisema kutokana na mashindano hayo yatafungua fursa kwa vijana kupata ajira katika vilabu vikubwa ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka wananchi kuachana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya ngono zembe ili kuzuia na kupunguza magonjwa yanayosababishwa na maambukizi na badala yake kupata muda zaidi kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa mbalimbali.
Michezo hiyo inatarajia kuendelea kufanyika kwa muda wa mwezi mmoja ndani ya manispaa ya Shinyanga ambapo kwa mshindi wa mchezo wa miguu atapokea zawadi ta Tshs milioni sita, kombe, seti ya jezi, pamoja na Mpira, mshindi wa pili milioni tatu , seti ya jezi pamoja na mpira, huku mshindi wa tatu atapokea kitita cha milioni moja, seti ya jezi, pamoja na Mpira huku mfungaji bora wa mashindano hayo atapokea zawadi ya Tsh Elfu hamsini, na Kwa mchezo wa dansi (dancing) mshindi atapata milioni moja.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga