- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NAIBU Katibu Mkuu wa ELIMU, Mhe. Dkt. Charles Msonde, pamoja na Mkurugenzi wa Elimu, Vicent Mkayombo wote kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), wametembelea Shule ya Msingi Mwalugoye iliyo ndani ya Kata ya Chibe katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi hao wamefanya ziara hiyo ili kuona Ujenzi wa madarasa ya mfano ya ELIMU YA AWALI na kupokea taarifa ya ujenzi wa madarasa hayo kutoka kwa Mwalimu Mkuu, Peter Bangili juu ya mchakato mzima wa Ujenzi wa Shule hiyo.
Baada ya kupokea taarifa hiyo, Dkt. Msonde ametoa pongezi kwa namna mchakato wa Ujenzi wa madarasa hayo ulivyofikia, akieleza kuwa majengo yamejengwa kwa kuzingatia ubora unaotakiwa.
“Nitoe pongezi zangu kwa Manispaa ya Shinyanga kwa hatua mliyofikia katika ujenzi huu, majengo yamekaa katika ubora ambao unatakiwa na kinachotakiwa ni kuhakikisha mapungufu yote yanayoonekana yaweze kufanyiwa kazi ili kila kitu kikamilike kwa asilimia 100”, amesema Dkt. Msonde.
Katika hatua nyingine Dkt. Msonde ametoa maagizo kwa Watendaji na Wasimamizi wa Elimu katika Manispaa ya Shinyanga kuhakikisha vifaa vyote muhimu vinakuwepo ikiwemo SimTank, Fire Extinguisher, Samani pia na kusawazisha vifusi ambavyo vilimwagwa eneo la Shule ili kuweka mandhari nzuri.
Aidha, Dkt. Msonde ameahidi kuitembelea tena Manispaa ya Shinyanga, kuja kushuhudia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga