- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MWL. KAGUNZE AONGOZA KONGAMANO LA WALIMU SPESHO MANISPAA YA SHINYANGA.
Na: Shinyanga Mc
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 21 Julai, 2025 ameongoza kongamano la walimu spesho lililoandaliwa na benki ya NMB kwa kujumuisha walimu kutoka shule mbalimbali za Manispaa ya shinyanga na Wilaya ya Shinyanga katika ukumbi wa makindo uliopo manispaa ya shinyanga.
Akiongea katika kongamano hili Mwl. Kagunze amewapongeza NMB kwa kutambua mchango mkubwa wa walimu katika kuleta maendeleo katika jamiii na kuwaomba walimu kuendelea kuwa walezi wazuri kwa watoto, huku akiwata kutumia fursa hii kujifunza mambo mbalimbali ya kifursa ikiwemo elimu ya fedha.
“Niwapongeze NMB kwa kutambua mchango mkubwa wa walimu katika jamii yetu, lakini pia niwapongeza walimu wote kwa juhudi kubwa mnazozifanya katika kuleta maendelea katika jamii yetu, niwaombe walimu kupitia kongamano hili jifunzeni fursa mbalimbali ikiwemo elimu ya fedha”. Amesema Mwl. Kagunze
Awali akiongea katika kongamano hili meneja mwandamizi wa idara ya wateja binafsi wa benki ya Nmb Ndg. Zuberi Rani ameeleza imekuwa ni desturi ya benki kuandaa kongamano la walimu kwa kutambua juhudi zao kwenye jamii kwa kuwalea na kuelimisha watoto,hivyo wanakutana na kuzungumza na walimu kwa kuzijadili fursa mbalimbali kwa kuwapatia elimu ya fedha.
Katika kongamano hili la walimu spesho walimu walipata wasaa wa kupata elimu ya mada ya afya ya akili, elimu ya ujasiliamali, elimu ya bima pamoja na elimu ya kutumia mfumo wa kiserikali (ESS) kwa ajili masuluhisho ya kifedha.
Kangamano la walimu spesho limeambatana na kauli mbiu isemayo Mwalimu Spesho - Umetufunza,Tunakutunza.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga