- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MWL. KAGUNZE AFUNGA MAFUNZO ELEKEZI YA KIELETRONIKI YA MFUMO WA MUKI.
Na. Shinyanga MC
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 16 Septemba, 2023 amefunga mafunzo elekezi ya kieletroniki MUKI yaliyoendeshwa kwa siku 2 kuanzia tarehe 15 hadi 16 Septemba, 2023 kwa Watumishi wa Manispaa katika ukumbi wa Shule ya Msingi Buhangija kata ya Ibinzamata.
Akizungumza katika kufunga mafunzo hayo Mwl. Kagunze amewataka Watumishi wakatumie mfumo wa MUKI katika kujifunza na kujikumbushia maswala ya kiutumishi ili kuzidi kuelewa zaidi Kanuni na Maadili ya Utumishi wa Umma .
"Mfumo huu wa MUKI mkautumie katika kujifunza mambo ya kiutumishi ili kuzidi kujua kanuni na maadili ya utumishi wa Umma pamoja na sheria mbalimbali muda wowote na wakati wowote kwani ni mfumo wa kieletroniki" alisema Mwl. Kagunze
Pamoja na mambo mengine Mwl. Kagunze amewakumbusha watumishi majukumu mbalimbali wanapofanya kazi zao za kila siku ikiwemo kusimamia Miradi ya Maendeleo,ukusanyaji wa mapato pamoja kuwasomea mapato na matumizi.
Mfumo MUKI unakwenda kurahisishia Watumishi wa Umma katika kujifunza mambo mbalimbali ya kiutumishi kwa njia ya kieletroniki kwa muda wowote na mahali popote.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga