- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MWL. KAGUNZE AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA YA KUKAGUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO PAMOJA NA VYANZO VYA MAPATO YA NDANI MANISPAA YA SHINYANGA
Na. Shinyanga MC
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius kagunze leo tarehe 18 Novemba, 2023 amefanya ziara ya kushtukiza ya Kukagua na kutembelea miradi mbalimbali pamoja na vyanzo vya Mapato ya ndani.
Mwl. Kagunze ametembelea miradi inayoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kujionea hatua za ujenzi zilipofikia huku akiwataka mafundi kuongeza kasi ya ujenzi na kuwa wazalendo katika kazi.
" Niwatake kuongeza kasi katika ujenzi ili muweze kumaliza kwa muda uliopangwa na majengo yaanze kutumika, pamoja na kuzidi kuwa wazalendo, kwani uzalendo katika kazi unaleta ufanisi wenye ubora " amesema Mwl. Kagunze
Aidha, miradi ya maendeleo ambayo ameweza kutembelea Mwl. Kagunze ni ujenzi wa shule ya sekondari Ngokolo B, ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya wasichana Shinyanga, ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi kata ya Lubaga pamoja na ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Idara kata ya Ndembezi.
Pamoja na mambo mengi Mwl. Kagunze alipata wasaa wa kutembelea vyanzo vya mapato ya ndani ikiwemo, soko kuu la Mitumba Ngokolo pamoja na Machinjio ya kisasa ya Mkoa katika kata ya Ndembezi,
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga