- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenge wa uhuru ukiendelea na uzindu na uwekaji wa mawe ya Msingi Katika miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Shinyanga umeweza kuweka pia klabu ya wapinga Rushwa Katika shule ya Sekondari Uhuru.
Akizindua klabu hiyo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Mwaka 2025 amefurahishwa na wimbo maalumu wa kupinga Rushwa kutoka kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Uhuru “RUSHWA NI ADUI WA HAKI” ambapo ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro kuwawezesha wanafunzi hao kuingia studio na kurekodi wimbo huo maalumu ili uweze kutoa Elimu juu ya athari za Rushwa hususani wakati huu wa Kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
“Binafsi nimejisikia Faraja kusikia vijana hawa wanachukia Rushwa, kwa wimbo wao walioimba hapa ni vizuri zaidi kama wangeenda studio ili kurekodi wimbo huu ili uwe kwa taifa zima juu ya athari za rushwa hususani wakati huu wa uchaguzi. Amesema Ndg Ussi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze Kuhakikisha wanafunzi hao wanarekondi wimbo huo kabla ya Agosti 30, 2025.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga