- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenge wa uhuru halmashauri ya manispaa ya shinyanga umeweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya machinga na bodaboda manispaa ya shinyanga mradi uliopo kata ya Lubaga mradi unaogharimu jumla ya Milioni 45,000,000 mpaka kukamilika kwake.
Akizungumza kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Mwaka ,2025 Ndg. Ismail Ali Ussi amesema ujenzi wa ofisi hiyo utaenda kurahisisha utoaji wa huduma kwa Bodaboda na Machinga wote waliopo ndani ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni pamoja na kurahisisha utoaji wa huduma sambamba na kurahisisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Katika hatua nyingine Ndg. Ussi amewasihi wakazi wa kata ya Lubaga kujitokeza kushiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 ili kupata viongozi bora kwa Mustakabari wa taifa letu.
Mbio za Mwenge wa uhuru Mwaka 2025 zinaongozwa na Kaulimbiu isemayo :Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga