- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kiongozi wa Mbio Mbio za mwenge wa uhuru 2025 Ndg. Ismail Ali Ussi amewapongeza wakazi wa kijiji Cha Mwamagunguli kwa kubuni na kuanzisha Ujenzi wa Zahanati ya kijiji kwa Nguvu zao ili kujiletea huduma wenyewe.
Ndg. Ussi ametoa Pongezi hizi Leo wakati akifungua zahanati ya kijiji Cha Mwamagunguli kata ya Kolandoto Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
“Niwapongeze sana wananchi kwa kubuni mradi huu ili kujisogezea huduma wenyewe, lakini pia nipongeze ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa kwa kutambua juhudi na adha ambayo walikuwa wakipitia wananchi hawa na kutenga Fedha kwa ajili ya kumalizia na kuboresha zaidi mazingira ya kutolewa huduma, niwasihi tu wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano wadaktari hawa ili waendelee kutoa huduma bora kwa wananchi” amesema Ndg. Ussi
Ujenzi wa Zahanati ya Mwamagunguli umegharimu kiasi cha Tsh milioni 140.
Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru 2025
“Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu “
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga