- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenge wa uhuru umeridhishwa na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Ishigwandama kata ya Kizumbi manispaa ya shinyanga wenye jumla ya shilingi milioni 106,890,563 ambapo mwenge wa uhuru umezundua mradi huo.
Akizungumza katika ufunguzi wa Shule hiyo kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2025 ndg. Ismail Ali Ussi amesema Wameridhishwa na ubora wa mradi huo ambapo ameipongeza halmashauri kwa usimamizi mzuri kwa kuzingatia ubora na viwango katika mradi huo.
“Mhe. Rais kwenye sekta hii ya Elimu ameitendea haki, Shule hii haina utofauti na shule iliyopo Jiji la Dodoma, na Dar es salaam viwago vilivyotumika kujenga shule hii ndivyo hivyo hivyo Katika Jiji la Dodoma kiukweli Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga hongereni sana kwa kuendelea kusimamia Fedha na Mradi huu umetekelezwa kikamilifu, Pongezi zangu za dhati kwa Mkurugenzi wa Manispaa kwa namna ambavyo kasimamia matumizi sahihi ya fedha kwa ujenzi wa shule hii na kwa ubora unaokubalika kiukwel Katika mradi huu mmemtendea haki Dkt. Samia, Sisi tumekagua kwa kina Ujenzi wa shule hii na Mwenge wa uhuru Umeridhishwa kufungua shule hii.
Mradi wa shule ya sekondari Ishigwandama umelega kuondoa changamoto ya wanafunzi kusafiri umbali mrefu ambapo ilikuwa ikiwakwamisha wanafunzi wengi kushindwa kufikia ndoto zao.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga