- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MANISPAA YA SHINYANGA MWL.ALEXIUS KAGUNZE AWAAPISHA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA.
NA. SHINYANGA MC
MSIMAMIZI wa uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amewaapisha jumla ya wasimamizi wa vituo vya Kupigia kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 570, kiapo cha kutunza siri pamoja na kiapo cha utii na uadilifu leo Novemba 24, 2025 Katika ukimbi wa mikutano Shule ya Sekondari Wasichana iliyopo kata ya Ndembezi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza baada ya kuwaapisha viapo hivyo Mwl. Kagunze amewata wasimamizi hao kuzingatia viapo hivyo kama walivyo apa.
“Jinsi mlivyo apa Leo kiapo Cha uamunifu na uadilifu ndivyo hivyo nendeni mkavitendee kazi viapo hivi, mmeteuliwa si kwa bahati mbaya bali serikali inaimani kubwa sana na ninyi, endapo mtakiuka viapo hivi hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yenu”. amesema Mwl. Kagunze
Kwa upande wake msaidizi wa uchaguzi halmashauri ya manispaa ya shinyanga Ndg. Charles Kafutila ameeleza kwamba waliojiandikisha kwenye daftari la wakazi wa eneo husika ndio watakao ruhusiwa kupika kura akiwa eno hilo na kwamba hataruhusiwa mtu kupiga kura nje ya eneo la makazi yake au kama hayupo kwenye orodha ya wakazi husika, na hatoruhusiwa kuingia na simu ya mkononi kwenye chumba cha kupigia kura.
Katika hatua nyingine Ndg. Kafutila amesema vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili kamili asubuhi(2:00) na kufungwa saa kumi kamili jioni (10:00) hivyo haitaruhusiwa kwa mtu yoyote kupiga kura nje au baada ya muda elekezi.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika jumatano ya Novemba 27,2024 ambapo Manispaa ya Shinyanga ina kata 17, vijiji 17, vitongoji 84 na mitaa 55,Viogozi watakaochaguliwa kupitia uchaguzi huo wa Serikali za mitaa ni pamoja na Wenyeviti wa Mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na wajumbe wao.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga