- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MSIKATISHWE NDOTO ZENU, ELIMU YENU IWE CHACHU YA MAENDELEO YA TAIFA”. RC MACHA
Na. Shinyanga MC
“ELIMU YENU IWE CHACHU YA MAENDELEO YA TAIFA”
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili kufanikisha ndoto zao na kujiandaa kuwa viongozi wa Taifa la kesho.
RC Macha ameyasema haya leo Mei 16, 2025, wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha sita katika Shule ya Wasichana Shinyanga iliyopo Manispaa ya Shinyanga, ambapo ametumia fursa hiyo kuwasihi wahitimu pamoja na wanafunzi wengine kuhakikisha hawakati tamaa wala kuruhusu ndoto zao kuvurugwa na vishawishi mbalimbali.
“Malipo pekee ya kuilipa serikali ni matokeo yenu mazuri katika mitihani mliyofanya. Shule kama hizi zipo katika mikoa 26 tu nchini Tanzania. Nia ya serikali ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira bora na salama. Elimu mliyopata hapa iende kuwa chachu ya maendeleo ya taifa letu. Ni imani yetu kwamba nyote mtaendelea na masomo ya vyuo vikuu kwa sababu mmelelewa na kufunzwa vyema,” amesema RC Macha.
Kwa upande wake, Afisa Elimu wa Sekondari Mkoa wa Shinyanga, Mwalimu Samson Hango, amempongeza Mkuu wa Shule hiyo kwa usimamizi bora wa maadili na nidhamu uliohakikisha kuwa wanafunzi wote 73 walioanza kidato cha tano wanahitimu salama.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Alexius Kagunze, ameeleza kuwa jitihada zinazofanywa na serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa kike na kufundishia kwa walimu ndizo zimechangia mafanikio haya.
Katika hatua nyingine, Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga imemtunuku Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Nurah Kamuntu, cheti cha pongezi pamoja na zawadi ya fedha taslimu shilingi 1,000,000/= kwa kutambua juhudi, mchango, uadilifu na moyo wake wa kujituma katika uongozi wa shule hiyo.
Shule ya Wasichana Shinyanga ni miongoni mwa shule 26 maalum za wasichana nchini, iliyoanzishwa mwaka 2023 kwa ajili ya Tahasusi za Sayansi. Hivi sasa shule ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu pamoja na kidato cha tano
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga