- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kanisa la International Evangelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT) limetoa Cheti cha pongezi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Jomaary Satura na kwa Watumishi wote wa Manispaa kutokana na kupiga hatua kubwa za Kimaendeleo yanayofanyika ndani ya Manispaa.
Cheti kilichotolewa na Kanisa na IEAGT kwenda kwa Mkurugenzi na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Akitoa vyeti hivyo vya pongezi, Ijumaa ya Oktoba 21 2022, Askofu wa Kanisa la IEAGT, David Mabushi kwa niaba ya Kanisa, amesema dhumuni la kutoa Cheti dhamira ni kumpongeza Mkurugenzi na Watumishi wote wanaoshirikiana naye katika kufanya maendeleo mbalimbali.
"Tumejionea wenyewe maendeleo yanayofanyika katika Manispaa yetu, hivyo tumeona tutoe vyeti vya pongezi kwa Mkurugenzi huyu anayesimamia maendeleo haya sambamba na Watumishi wengine anaoshirikiana nao.
"Kuna mabadiliko makubwa sana kwa Manispaa yetu ya kimaendeleo, ambayo hayajawahi tokea, na huu ndio Utumishi uliotukuka hivyo hatuna budi kupongeza" amesema Mabushi.
Kwa upande wake Dkt. Satura baada ya kupokea vyeti vya pongezi, amesema katika maisha yake hajawahi kupewa pongezi na viongozi wa kiroho, hivyo alichofanyiwa ni muujiza mkubwa katika maisha yake.
Dkt. Satura ameahidi kufanya mambo makubwa zaidi katika Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na watumishi wenzake.
"Huu ni muujiza mkubwa kwangu, haujawahi kutokea hivyo najikuta naandika historia yangu hii kutokana na ushirikiano wa watumishi wenzangu.
"Nawashukuru sana viongozi wangu wa kiroho, nimekuwa nikipata pongezi kutoka kwa wananchi kwa kupigiwa simu, lakini hiki mlichonifanyia leo nakithamini sana, namrudishia Sifa na Utukufu Mwenyezi Mungu, na kwa niaba ya wenzangu, tunaahidi kufanya makubwa zaidi na hii ni hatua ya awali tu" amesema Satura.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga