- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shinyanga MC.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christiana Solomon Mndeme leo tarehe 26 Aprili, 2023 ameongoza wana Shinyanga katika kuadhimisha sherehe za mika 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuzindua Zahanati ya Masekelo iliyopo Kata ya Masekelo Katika Manispaa ya Shinyanga huku akiwataka wananchi wa Kata hiyo kuhakikisha inatunzwa ili inufaishe na vizazi vijavyo.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Zahanati hiyo, Mhe. Mndeme aliwaambia wananchi hao kuwa ni muhimu sana kuendelea kujivunia Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar kwakuwa ndiyo umeweza kuwakutanisha leo katika tukio hilo muhimu kabisa la uzinduzi wa Zahanati ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Çhama Cha Mapinduzi (2020) ambacho kilizaliwa kutoka katika Muungano ambao leo una miaka 59.
"Ndugu zangu wananchi, leo yupo hapa kwenye tukio muhimu kabisa tena linalohusu afya za watu wetu tukiwa na amani, upendo, mshikamano na udugu wetu huu mnaouona ni matunda ya Muungano ulioasisiwa na viongozi wetu Sheikh Abeid Amani Karume aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Mwl Julius Nyerere aliyekuwa Rais wa Tanganyika wakati huo. Hivyo ni muhimu sana kwetu sisi tunapokwenda kuadhimisha sherehe hizi tuuenzi Muungano wetu, tuwaenzi waasisi wa Muungano kwa kudumisha upendo, amani na mshikamano," alisema Mhe. Mndeme.
Awali akifungua maadhimisho hayo katika viwanja vya Zimamoto aliwahutubia wananchi waliokuwa wamejaa uwanjani hapo kuwa, Shinyanga inajivunia Muungano kwakuwa imepiga hatua kubwa sana katika nyanja mbalimbali ikiwamo Elimu, Afya, Miundomniju, ustawi wa wananchi kiuchumi nk.
Pamoja na mafanikio lukuki yaliyopatikana ndani ya miaka 59 ya Muungano, lakini Mkoa wa Shinyanga umepiga hatua kubwa sana katika Elimu ambapo miaka 59 iliyopita mpaka sasa Shinyanga ina jumla ya shule 646 huku akielezea upande wa Afya kuwa miaka 59 iliyopita wa Shinyanga ilikuwa na Zahanati 10 tu, ambapo mpaka kufika leo kuna jumla ya Zahanati 250 ikiwamo na hii ya Masekelo ambayo itanufaisha wananchi 19332.
MATUKIO KATIKA PICHA
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga