- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, amezindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye Miradi ya Maendeleo Manispaa ya Shinyanga, na kushiriki ujenzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya Shinyanga.
Mwenge huo wa Uhuru umekimbizwa leo Julai 27,2022 katika Manispaa ya Shinyanga, ukitokea halmashauri ya Shinyanga, ambao umepitia Miradi Mitano ya Maendeleo na yote imekubaliwa.
Akizungumza wakati akikagua Miradi hiyo ya maendeleo kwa nyakati tofauti, Geraruma amesema Miradi yote ni mizuri na ameridhia kuweka Mawe ya Msingi pamoja na kuizindua.
"Miradi yote ya maendeleo ambayo nimeipitia ni mizuri na ile ambayo nimetoa maelekezo ifanyiwe marekebisho na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi," amesema Geraruma.
Katika hatua nyingine, ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga siku ya Kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu, wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa.
Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye ulemavu, amepongeza usimamizi mzuri wa Miradi hiyo ya maendeleo na kutumia fedha vizuri ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Rajab Masanche, awali akipokea Mwenge huo wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Nice Munissy amesema Mwenge huo umezindua Miradi ya maendeleo Miwili ambayo ni Ujenzi wa Zahanati ya Bushushu iliyogharimu shilingi 110,913,660/= na Mradi wa Maji Bugwandege.
Amesema Mwenge huo pia umeweka Mawe ya Msingi katika Kiwanda cha Bia cha Gaki Investment Jengo la utawala la Manispaa ya Shinyanga litakalogharimu kiasi cha shilingi 2,400,000,000/=, ujenzi vyumba vya Madarasa Sita na Ofisi mbili za walimu katika Shule ya Msingi Ugweto vyenye gharama ya shilingi 112,500,000/=.
Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu (2022) inasema "Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo, Shiriki kuhesabiwa kwa Maendeleo ya Taifaā€¯.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga