- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Masumbuko, ametoa wito kwa Baraza la Madiwani manispaa ya shinyanga kushirikiana kwa karibu na vyombo vya dola pale panapojitokeza viashiria vya wizi wa vifaa vya ujenzi katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani ya halmashauri.
Mhe. Masumbuko ametoa wito huu leo Mei 07, 2025, katika kikao cha pili cha Baraza la Madiwani kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025 (Januari–Machi), kilichoketi kwa ajili ya kupokea taarifa za utekelezaji kutoka kwa Kamati za Kudumu za Halmashauri pamoja na taarifa kutoka taasisi za umma zikiwemo TANESCO, SHUWASA, na TARURA, pamoja na taarifa ya Mkurugenzi wa Manispaa.
“tushirikiane kikamilifu na vyombo vya dola, Diwani ndiye mwenyekiti wa kata husika, kata zetu haziwezi kuendelea endapo kama vifaa vinavyonunuliwa na serikali kwa ajili ya ujenzi au ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma kwa wananchi vitakiwa vinaibiwa, Ushirikiano wenu ni nguzo muhimu katika kulinda rasilimali za umma na kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kama ilivyokusudiwa.” Amesema Mhe. masumbuko
Viongozi wa taasisi hizo za umma wamewahakikishia wananchi kupitia Baraza la Madiwani kuwa wataendelea kuboresha miundombinu na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi, sambamba na malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, ametoa wito kwa Madiwani kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na faida zake, ili kuiwezesha Serikali kujenga na kuboresha miundombinu pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi kupitia mapato yao.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga