- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na. Shinyanga MC.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi ameitaka Manispaa ya Shinyanga kumalizia
ujenzi wa Zahanati ya Kata Kolandoto ili kuwaondolea adha wananchi wa Kata hiyo ya kutembea umbali
mrefu kufuata huduma ya matibabu.
Mhe. Johati ameyasema hayo leo tarehe 9 Mei, 2023 kwenye mkutano wa na wananchi wa Kata ya
Kolandoto wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya
Shinyanga baada ya kusomewa taarifa utekelezaji na wananchi kutoa ombi hilo kwake kwamba ujenzi
wa Zahanati hiyo umechukua muda mrefu sana kuanzia mwaka 2010.
"Nimepokea taarifa yenu ya utekelezaji wa miradi, lakini kwenye hili ombi ambalo limetolewa na
wananchi hawa wa Kata ya Kolandoto naomba lichukuliwe kwa uzito na umuhimu wa aina yake, uzuri ni
kwamba Mkurugenzi wa Manispaa upo hapa na Mstahiki Meya wa Manispaa upo hapa pia, niwaombe
mkapitishe bajeti kwa mwakwa wa fedha 2023/2024 ya umaliziaji wa Zahanati hii ambayo ni muhimu
kwa wananchi wetu ukizingatia kuwa imekuwa ya muda mrefu sana ili kero hii ya wananchi ifikie mwisho
sasa mwaka huu," alisema Mhe. Johari.
Katika mkutano huo wa hadhara wananchi walieleza kero zao na kutoa maombi yao ikiwa ni pamoja na
kuomba kufanyika kwa ukarabati wa shule ya msingi Kolandoto ambayo ilijengwa yangu mwaka 1962
kwa sasa inauo majengo yaliyochoka, kupelekwa kwa Mtendaji katika Kijiji cha Galamba, kupatiwa
ufumbuzi wa malalamiko ya waliofanyiwa uthamini kupisha uendelezaji wa mradi wa Uwanja wa Ndege
walipwe stahiki zao, kupelekewa huduma ya umeme kwa kijiji cha Galamba, na maji kwa baadhi ya vijiji
vya Mwabahabi na Msumbiji.
Hoja hizo zilipatiwa majibu na viongozi mbalimbali walioambatana na Mhe. Johari ambapo suala la
Mtendaji wa kijiji Mkurugenzi wa Manispaa aliahidi kumpeleka huku akiwasihi wananchi kuacha tabia ya
kukataa watumishi, kuhusu maji Mhe. Mussa Elias Diwani Kata ya Kolandoto alisema Kolandoto ipo
kwenye mpango wa kupelekewa huduma hiyo, na suala la fidia Mhe. Johari alisema hakuna mwananchi
atakayedhurumiwa haki yake.
Hii ni siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili katika Manispaa itakayotekelezwa na Mhe. Johari ikiwa ni
sehemu ya utaratibu wake wa kukagua utekelezaji wa miradi pamoja na kufanya mikutano ya hadhara
kwa lenho la kupokea changamoto zinazowakabili wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Mhe. Johari aliyevaa Kilemba chekundu akiendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Kata ya Kolandoto, hilo ni jengo la vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Kolandoto
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga