- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MHE JERRY SILAA AKUTANA NA WATUMISHI SEKTA YA ARDHI MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa leo tarehe 4 Novemba, 2023 amekutana na Watumishi wa Sekta ya ardhi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza katika kikao Mhe. Silaa amewataka watumishi wa sekta ya ardhi kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi katika kutatua migogoro ya ardhi huku akiwasihi siku Rais akifanya ziara katika Mkoa wa Shinyanga asipokelewe na Mabango ya migogoro ya ardhi bali apokelewa kwa furaha na shangwe.
"Kazi niliyopewa kufanya na Rais Mhe.Samia ni kuhakikisha kwamba siku akifanya ziara hapa Shinyanga akipita barabarani wananchi wawe wanampungia mikono, ni fedheha kubwa anapokuja kwenye ziara Mheshimiwa Rais badala ya wananchi kumpungia mikono kwa furaha wanashika Mabango, kushika kwao Mabango ina maana kwamba sisi aliotupa dhamana kumsaidia hutufanya kazi yetu" amema Mhe. Silaha
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema serikali mkoani Shinyanga itaendelea kusimamia suala la mipango miji pamoja na matumizi bora ya ardhi ili kuzuia matatizo ya Migogoro ya ardhi yasiendelee kuibuka.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga