• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Fedha
      • Ujenzi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Hearth
      • Usafi na Mazingira
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Tecknolojia, Habari, Mawasiliano na Uhusiano
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Nyuki na Maliasili
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uwekezaji wa Viwanda
    • Fursa za kilimo
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Fursa za elimu
    • Fursa za Afya
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma ya utoaji wa Mikopo
    • Kukondisha Vyumba vya Biashara
    • Unyonyaji wa Maji Taka
    • Huduma za Biashara
      • Leseni za Biashara
      • Elimu ya kibiashara
      • Ukaguzi wa Viwanda
      • Usimamizi wa Masoko
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Miundombinu
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya kamati za Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iIliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Mafunzo

MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI WAZINDULIWA RASMI MKOA WA SHINYANGA

Posted on: February 20th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amezindua Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga kwa kuweka Vibao vya Maelekezo ya Mtaa wa Barabara ya Uhuru (Uhuru Road) na Mtaa wa Market pamoja na Namba za Majengo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Manispaa ya Shinyanga huku akisisitiza kuwa zoezi hilo linatakiwa likamilike ifikapo mwezi Aprili 2022 katika mitaa yote mkoani Shinyanga.

Uzinduzi wa Mfumo wa Anwani za Makazi unaohusisha uwekaji mabango (vibao) ya maelezo ya mtaa, uwekaji namba kwenye nyumba na taarifa za ndani ya nyumba umefanyika  Ijumaa Februari 18,2022 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri zote sita za mkoa wa Shinyanga likishuhudiwa na wananchi Mjini Shinyanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Mjema amesema uzinduzi wa Mtaa wa Sokoni katika Manispaa ya Shinyanga unawakilisha mitaa yote katika mkoa wa Shinyanga akibainisha kuwa mfumo wa Anuani za Makazi utasaidia kuwatambua wananchi hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali katika jamii.

“Zoezi hili la kutambua makazi linatakiwa likamilike hadi ifikapo mwezi Aprili mwaka huu. Anuani za Makazi utasaidia kuwahudumia wananchi kwa ufanisi. Mwaka huu zoezi la Sensa litafanyika kikamilifu kwani itakuwa ni Sensa ya Watu na Makazi. Hii itakuwa tofauti na miaka ya nyuma kidogo ambapo tumekuwa na Sensa ya watu pekee bila makazi yao. Anuani za Makazi zitarahisisha zoezi hili kwani Sensa itahusisha kujua idadi ya wakazi, nyumba zao na kutambua mitaa yao”,amesema Mjema.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amewataka wananchi kutunza alama hizo za utambuzi wa makazi kwani zitasaidia kurahisisha kutambua mitaa na nyumba za wananchi.

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati aliyevaa kilemba) baada ya kuzindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga kwa kuweka Vibao vya Maelekezo ya Mtaa wa Market na Barabara ya Uhuru Road katika Manispaa ya Shinyanga. 

 

 

Muonekano wa Maandishi ya upande wa pili wa Vibao vya Maelekezo ya Mtaa wa Market na Uhuru Road katika Manispaa ya Shinyanga.

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  Ijumaa Februari 18,2022. 

 

 

Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  Ijumaa Februari 18,2022. 

 

 

 

Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Ibrahim Kiyungu akizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuzindua Namba 28 ya Jengo la TANESCO wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  Ijumaa Februari 18,2022. 

 

 

Namba 28 ya Jengo la TANESCO 

 

 

Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Pendolake Msangi akizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuzindua Namba 32 ya Jengo la TANESCO wakati akizindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga Ijumaa Februari 18,2022. 

 

 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuzindua rasmi Mfumo wa Anwani za Makazi mkoa wa Shinyanga  Ijumaa Februari 18,2022. 

  

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • Tazama

Habari Mpya

  • ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    May 08, 2025
  • MHE.MASUMBUKO AWATAKA MADIWANI KUSHIRIKIANA KIKAMILIFU KUKABILIANA NA WIZI WA VIFAA VYA MIRADI YA MAENDELEO.

    May 07, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MAAGIZO

    May 06, 2025
  • SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA SHULE YA WASICHANA SHINYANGA ILI KUIFANYA KUWA MIONGONI MWA SHULE BORA NCHINI “. NDG. MSIGWA.

    May 03, 2025
  • Tazama

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
Video Zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Ripoti mbalimbali
  • Sheria Ndogondogo za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Tovuti Nyingine tunazohusiana

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa(TAMISEM)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknologia
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Mkoa wa Shinyanga
  • Sekretarieti ya Ajira

wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Tanesco S, Mwanza Road

    Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga

    Simu: +255-28-2763213

    Simu ya Mkononi: 0759 023 788

    Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Ramani ya Tovuti
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga