- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MENEJIMENTI YA MANISPAA YA SHINYANGA YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.
Na: SHINYANGA MC
Menejimenti ya Manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na muwakilishi wa mkurugenzi Ndg. Jackson Mwakisu ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu Manispaa ya Shinyanga wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani Manispaa ya shinyanga leo tarehe 15, Julai 2025.
Akizungumza katika ziara hii Ndg. mwakisu amewata mafundi kuongeza kasi ya ujenzi pamoja na kujenga majengo yenye ubora kulingana na thamani ya fedhaviliyotolewa na serikali.
“Ongezeni kasi ya ujenzi na uwe ujenzi wenye kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali ili majengo haya yaanza kutumika kwa wanufaika wa miradi hii”. Amesema Ndg. Mwakisu
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni Ujenzi wa shule mpya ya ishigwandama iliyopo kata ya kizumbi, Ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi ilwelyangula kata ya kitangiri, Ujenzi wa ofisi ya wajisiriamali kata ya lubaga, Ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi kambarage kata ya kambarage, Ujenzi wa zahanati mwamagunguli kata ya kolandoto pamoja na ujenzi wa mabweni 4 na matundu ya vyoo 12 katikabshule ya sekondari Rajani kata ya Ibadakuli.
Lengo la ziara hii ni kuangalia hatua ipi imefikia ya utekelezaji wa Miradi pamoja na kutilia nguvu pale palipokuwa na changamoto na kutoa ushauri wa mambo mbalimbali.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga