- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Menejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ubora unaotakiwa, imefanya ziara ya kutembelea na kukagua jumla ya miradi mitatu inayotekelezwa katika kata mbalimbali za Manispaa ya Shinyanga.
Katika ziara hii iliyofanyika leo Aprili 09,2025 menejimenti ya manispaa ya shinyanga imekagua ujenzi wa jengo la utawala la Manispaa ya Shinyanga linalotekelezwa katika kata ya Chamaguha, jengo linatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni 2025 , aidha menejimenti imekagua ujenzi wa mabweni manne na matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Rajani, kata ya Ibadakuli, mradi ambao una thamani ya Tshs Milioni 570,000,000/= , ambapo ujenzi huu unakusudia kuboresha mazingira ya shule hiyo na kutoa huduma bora kwa wanafunzi, pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari katika kata ya Kizumbi, yenye gharama ya Tshs Milioni 103,000,000, mradi ambao unalenga kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi wa maeneo hayo.
Wakizungumza katika ziara hii, menejimenti imetoa wito kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi hii kwa kuhakikisha wanazingatia ubora wa majengo kilingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali, huku ikisisitiza kuwa miradi yote inatakiwa kukamilika kwa wakati na kwa viwango vya juu ili kutoa matokeo bora kwa jamii, na kuanza kutumika kwa wanafunzi ambao watafaidika na miundombinu hii.
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi, huku ikizingatia umuhimu wa kuboresha sekta ya elimu na miundombinu ili kupunguza changamoto zinazowakabili wananchi, hasa wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kutafuta elimu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga