• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Fedha
      • Ujenzi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Hearth
      • Usafi na Mazingira
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Tecknolojia, Habari, Mawasiliano na Uhusiano
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Nyuki na Maliasili
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uwekezaji wa Viwanda
    • Fursa za kilimo
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Fursa za elimu
    • Fursa za Afya
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma ya utoaji wa Mikopo
    • Kukondisha Vyumba vya Biashara
    • Unyonyaji wa Maji Taka
    • Huduma za Biashara
      • Leseni za Biashara
      • Elimu ya kibiashara
      • Ukaguzi wa Viwanda
      • Usimamizi wa Masoko
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Miundombinu
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya kamati za Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iIliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Mafunzo

MANISPAA YA SHINYANGA YAZINDUA DAWATI LA USTAWI WA JAMII KUKABILIANA NA UKATILI STANDI YA MABASI MKOA WA SHINYANGA.

Posted on: June 20th, 2025

Katika kuunga mkono juhudi za serikali juu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili na kusaidia watoto wanaoishi mitaani, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kwa kushirikiana na shirika la Railway Children Africa, imezindua rasmi Dawati la Ustawi wa Jamii katika Stendi ya Mabasi ya Mkoa wa Shinyanga.


Akizungumza haya leo juni 20, 2025 katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Neema Rwegoshola, amelipongeza shirika hilo kwa juhudi kubwa za kuwajali watoto waishio mitaani huku akisisitiza kuwa kila mwananchi ana wajibu wa kushirikiana na mradi huu ili kusaidia kupunguza ongezeko la watoto hao na kujenga taifa imara la baadaye.


“Tunapaswa kushikamana kama jamii na kuhakikisha watoto hawa wanapata msaada wanaouhitaji. Uwepo wa dawati hili utarahisisha utoaji wa huduma muhimu za ustawi wa jamii na kuwa daraja la matumaini kwa watoto walio katika mazingira magumu hususani eneo hili la standi,” amesema Bi. Rwegoshola.


Kwa upande wake, Meneja wa Mradi kutoka Shirika la Railway Children Africa, Bi. Irene Wampembe, amesema kuwa uanzishwaji wa ofisi hiyo ndani ya standi ni mkakati mahususi wa kufikisha huduma karibu zaidi na wananchi na kuwasaidia watoto wanaoishi mitaani huku akiongeza kuwa lengo ni kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia, kuhamasisha malezi bora, na kufanikisha jitihada za kutokomeza vitendo vya kikatili na unyanyasaji.


Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Revocatus Rutunda, amesema halmashauri itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha vitendo vya ukatili vinatokomezwa kabisa ndani ya manispaa ya shinyanga huku akilipongeza Shirika hilo kwa utekelezaji wa mradi huo ndani ya manispaa.


Uzinduzi wa Ofisi hii ndani ya manispaa ya shinyanga ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya halmashauri katika kuhakikisha ustawi wa watoto na ustawi wa kijamii kwa ujumla unapata kipaumbele, hasa kwa wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • Tazama

Habari Mpya

  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • SALAMU ZA SHUKRANI

    June 24, 2025
  • Tazama

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
Video Zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Ripoti mbalimbali
  • Sheria Ndogondogo za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Tovuti Nyingine tunazohusiana

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa(TAMISEM)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknologia
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Mkoa wa Shinyanga
  • Sekretarieti ya Ajira

wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Tanesco S, Mwanza Road

    Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga

    Simu: +255-28-2763213

    Simu ya Mkononi: 0759 023 788

    Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Ramani ya Tovuti
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga