- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya manispaa ya shinyanga Katika kuadhimisha siku ya misitu sambamba na Siku ya upandaji miti kitaifa imepanda na kugawa jumla ya miche 1200 ya matunda na kimvuri katika soko la wazi mnada wa wajasiliamali wadogowadogo lililopo mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Halmashauri ya manispaa ya shinyanga.
Akizungumza katika zoezi hili la upandaji miti Mkuu wa Idara ya Maliasili na mazingira Manispaa ya Shinyanga Ndg. Ezra Manjerenga amesema kwa kutambua umuhimu wa utunzaji miti na mazingira uongozi wa manispaa ya shinyanga umepanda miti ya kimvuri na matunda katika eneo soko la wazi (MNADA) lililopo mtaa wa dome kata ya ndembezi huku akiwataka wananchi na wafanyabiashara kuitunza ili iweze kukua.
“Uongozi wa manispaa ya shinyanga katika kuadhimisha siku ya misitu duniani umeamua kupanda miti hii ya kimvuri na matunda katika eneo hili la mnada, rai yangu kwa wajasiliamali katika eneo hili tuitunze ili iweze kukua na kutoa matunda na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, lakini nitoe wito kwa wananchi wa manispaa ya shinyanga kufika ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya shinyanga kuchukua miche ya miti ambayo inatolewa bure”. Amesema Ndg. Majerega
Katika hatua nyingine Ndg. Manjerenga amesema manispaa ya shinyanga imetunga sheria ndogo ya usafi wa mazingira dhidi ya waharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo ambapo faini ni Tshs 50,000 hadi Tshs 300,000 au kifungo jela miezi sita.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga