- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamepitisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo jumla ya shilingi 40,271,905,280/= zinatarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali na zitatumika katika shughuli za utoaji huduma, utawala, na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mapendekezo haya yamewasilishwa katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika leo, Januari 30, 2025 huku madiwani wakikubaliana na bajeti hiyo na kutoa ushauri wa kuboresha baadhi ya maeneo, hasa kuhusu huduma ya maji safi na salama na ujenzi wa barabara kutokana na hali mbaya ya miundombinu ya barabara katika maeneo mengi.
Akitoa taarifa kuhusu Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hii kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Mensaria Mrema, amesema kuwa fedha zitakazokusanywa zinatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato, ikiwa ni pamoja na Vyanzo vya mapato ya ndani Shilingi 6,403,000,000/= na Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu Shilingi 6,497,592,000/= Vyanzo vingine ni Ruzuku ya matumizi mengineyo: Shilingi 1,357,940,000/=, Ruzuku ya mishahara: Shilingi 22,219,049,200/= na Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Wahisani: Shilingi 3,794,324,080/=.
Kwa upande Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Masumbuko, amesisitiza kuwa mapendekezo haya ni hatua ya mwanzo na madiwani bado wanaruhusiwa kutoa maoni kwa ajili ya marekebisho zaidi.
Agenda zilizowasilisha katika kikao ni pamoja na kupitia mapitio ya mpango wa bajeti ya mwaka 2023/2024, nusu ya mwaka wa fedha 2024/2025, mapendekezo ya mapato ya ndani kwa mwaka 2025/2026 na mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga