- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MADIWANI wa Manispaa ya Shinyanga wamewasilisha taarifa za kwenye Kata zao, huku wakibainisha changamoto ambazo bado zinawakabiliwa wananchi na kuhitaji kutatuliwa.
Wamewasilisha taarifa hizo leo Mei 10, 2022 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, ambacho kilikuwa na ajenda ya maswali ya papo kwa papo, kupokea na kujadili taarifa za kwenye Kata.
Madiwani hao kwa nyakati tofauti kila mmoja akiwasilisha taarifa ya kwenye Kata yake, walibainisha changamoto ambazo bado zinawakili wananchi ikiwamo ubovu wa miundombinu ya barabara, uchakavu majengo ya shule, matundu ya vyoo, kutokamilika ujenzi maboma ya Zahanati, kituo cha Polisi Ngokolo, upungufu wa madawati shule ya msingi Mapinduzi “B” Ngokolo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani, amesema changamoto zote ambazo zimewasilishwa na Madiwani kwenye taarifa zao zifanyiwe kazi.
Aidha, katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani walimpatia cheti cha Pongezi Mwananchi Saimon Kashinje mkazi wa kitongoji cha Mwamagulya Kata ya Oldshinyanga, kwa kutoa eneo bure Hekali Tano kwa ajili ya ujenzi shule Shikizi ya Mwamagulya.
Mkurugenzi wa Manispaa Jomaary Satura akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Diwani wa Kambarage Hassani Mwendapole akiwasilisha taarifa ya kwenye Kata yake.
Wataalam wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (katikati) akimpatia Cheti cha Pongezi Mwananchi Mashishanga Kashinje mkazi wa kitongoji cha Mwamagulya Oldshinyanga, kwa kutoa eneo bure kwa ajili ya ujenzi wa shule Shikizi ya Mwamagulya.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga