• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Fedha
      • Ujenzi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Hearth
      • Usafi na Mazingira
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Tecknolojia, Habari, Mawasiliano na Uhusiano
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Nyuki na Maliasili
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uwekezaji wa Viwanda
    • Fursa za kilimo
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Fursa za elimu
    • Fursa za Afya
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma ya utoaji wa Mikopo
    • Kukondisha Vyumba vya Biashara
    • Unyonyaji wa Maji Taka
    • Huduma za Biashara
      • Leseni za Biashara
      • Elimu ya kibiashara
      • Ukaguzi wa Viwanda
      • Usimamizi wa Masoko
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Miundombinu
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya kamati za Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iIliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Mafunzo

MADIWANI MANISPAA SHINYANGA WATOA TAMKO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO

Posted on: February 11th, 2023

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wametoa tamko la kulaani vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wadogo, ambavyo vinaendelea ndani ya jamii, yakiwemo matukio ya ubakaji na ulawiti.

Tamko hilo wamelitoa Februari 10, 2023 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wakati akichangia Taarifa ya Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu kilichofanyika katika Ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo Manispaa ya Shinyanga.

Wamesema matukio ya ukatili dhidi ya watoto Katika Manispaa ya Shinyanga yamekithiri, hivyo elimu inapaswa kuendelea kutolea kwa wananchi kuachana na vitendo hivyo ili kuto waathiri watoto kisaikolojia na kushindwa kutimiza ndoto zao.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Uchumi Afya na Elimu, Shela Mshandete, alisema inaumiza sana kuona watoto wadogo wakiendelea kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia, tena wakifanyiwa na watu ambao ni wa karibu.

“Tushikamane madiwani na kutoa Tamko la kulaani matukio ya ukatili dhidi ya watoto wadogo, na ajenda hii ya kupinga ukatili iwe ya kudumu tuzungumza kwenye mikutano yetu yote ikiwamo ya hadhara ili Shinyanga kusiwepo na ukatili tena,”amesema Shela.

“Tunaliomba pia Jeshi la Polisi kesi za ukatili zikifika kwenye dawati lao wazishughulikie kikamilifu ili wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria, na siyo kuzisuluhisha kimya kimya,”aliongeza.

Ametoa wito pia kwa wananchi kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake, ili kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili wasome na kutimiza ndoto zao.

Katika hatua nyingine alisisitiza suala la watoto kula chakula shuleni na kuwaomba wazazi wachangie chakula kila mmoja debe moja la unga na kilo 4 za sukari, ambapo mwanafunzi atakula mwaka mzima, na kusoma bila ya kuwa na njaa na hatimaye kufanya vizuri kitaaluma.

Aidha katika Baraza hilo ziliwasilishwa taarifa za Kamati ikiwamo Kamati ya Ukimwi, Kamati ya fedha na Utawala, na Kamati ya Uchumi Afya na Elimu, na kujadiliwa mambo mbalimbali ikiwamo upungufu wa matundu ya choo shuleni.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Jomaary Satura, akiwasilisha taarifa yake kwenye Baraza hilo, alieleza kuwa, changamoto zote ambazo zimewasilishwa watazifayika kazi na zingine zipo kwenye utekelezaji, huku akisisitiza kwamba hali ya mwenendo ya utendaji katika halmashauri inazidi kuimarika kutoka na kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji.

Satura aliongeza kwa kusema Halmashauri itaendelea na kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, fedha ambazo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • Tazama

Habari Mpya

  • ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    May 08, 2025
  • MHE.MASUMBUKO AWATAKA MADIWANI KUSHIRIKIANA KIKAMILIFU KUKABILIANA NA WIZI WA VIFAA VYA MIRADI YA MAENDELEO.

    May 07, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MAAGIZO

    May 06, 2025
  • SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA SHULE YA WASICHANA SHINYANGA ILI KUIFANYA KUWA MIONGONI MWA SHULE BORA NCHINI “. NDG. MSIGWA.

    May 03, 2025
  • Tazama

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
Video Zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Ripoti mbalimbali
  • Sheria Ndogondogo za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Tovuti Nyingine tunazohusiana

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa(TAMISEM)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknologia
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Mkoa wa Shinyanga
  • Sekretarieti ya Ajira

wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Tanesco S, Mwanza Road

    Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga

    Simu: +255-28-2763213

    Simu ya Mkononi: 0759 023 788

    Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Ramani ya Tovuti
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga