- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maafisa waandikishaji wasaidizi wa Jimbo la Uchaguzi Shinyanga Mjini leo Agosti 14,2024 wameapishwa na hakimu Agness Said Mlimbi kiapo cha kutunza siri Pamoja na kiapo cha kutofungamana na chama chochote cha siasa.
Mafunzo hayo na viapo hivyo vimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa lewis Kalinjuna uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa maafisa hao wasaidizi waandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Awali akitoa msisitizo Hakimu Mlimbi amewasihi maafisa wasaidizi hao kufanya kazi chini ya misingi na utaratibu
“Tume huru ya uchaguzi imewaamini kuwa mnaweza kufanya kazi chini ya misingi na taratibu”. amesema Hakimu Mlimbi
Kwa upande wake Afisa mwandikishaji jimbo la shinyanga Mjini Mwl. Alexius Kagunze amewataka maafisa waandikishaji wasaidizi Pamoja na waendeshaji vifaa vya bayometriki kuwa makini kusikiliza mafunzo hayo.
“zoezi hili sio la siasa,mimi kama afisa mwandikishaji sitowavumilia maafisa wasaidizi wavivu na ambao hawatakwenda na taratibu na kanunu za uchaguzi,zingatieni mafunzo haya,kuweni makini ili mkatende kazi kama ipasavyo”. amesema Mwl. Kagunze
Mafunzo haya yataendelea kwa siku mbili kwa lengo la kutoa mafunzo kwa maafisa waandikishaji wasaidizi watakaokwenda kusimamia Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura ambalo kwa jimbo la shinyanga Mjini zoezi hilo litaanza Agosti 21 hadi 27, 2024.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga