- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
SHIRIKISHO la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) mkoani Shinyanga, limeadhimisha siku ya wafanyakazi Mei mosi, huku likibainisha changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili watumishi wa umma na Sekta binafsi.
Maadhimisho yao yamefanyika leo Mei 1, 2022 katika viwanja vya michezo CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga, huku mgeni Rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.
Akihutubia kwenye Maadhimisho hayo, Mjema amewataka watumishi wa Serikali mkoani humo, kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kujituma, na kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu ili itekelezwe kwa ubora.
"Malipo kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan ni kufanya kazi kwa bidii na kutumikia wananchi ipasavyo pamoja na kusimamia vyema miradi ya kimkakati", alisema Mjema.
Aidha, aliwataka pia watumishi wa umma kulisimamia vyema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa weledi mkubwa, ambalo litafanyika Agosti 23 mwaka huu ili malengo yaliyokusudiwa yafanikiwe na kuwasihi wananchi wakati wa zoezi hilo wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa.
Katika hatua nyingine, alisema changamoto zote ambazo zimewasilishwa kwenye maadhimisho hayo, zile ambazo zipo ndani ya uwezo wake atazitafutia ufumbuzi, na zilizo nje ya uwezo wake za Kitaifa ataziwasilisha kwenye mamlaka husika.
Mjema pia alimwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, kushughulikia malalamiko yote ya Sekta binafsi juu ya wafanyakazi wao ndazi ya mwezi mmoja, ambayo yametolewa na Shirikisho hilo la vyama vya wafanyakazi (TUCTA), na watakaokaidi kutii maagizo ya Serikali watachuliwe hatua.
“Sekta binafsi inavyofanya juu ya wafanyakazi wao ni kinyume cha Sheria za ajira hili tutalishughulikia,”alisema Mjema.
Awali Mratibu wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Lazaro Mnjeja, akisoma Risala, alibainisha changamoto ambazo zinawakabili wafanyakazi wa Sekta binafsi, kuwa waajiri hawawapatii mikataba ya ajira, kuwazuia kujiunga na vyama vya wafanyakazi, hawapeleki michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na hawatoi hati za malipo ya mishahara.
Alitaja changamoto zingine ambazo zinawakabili pia na wafanyakazi wa Sekta za umma na binafsi, kuwa ni ucheleweshwaji wa mafao kwa wastaafu, kutolipwa madai ya Likizo, uhamisho, kutopandishwa madaraja na mapunjo ya mishahara.
Pia aliiomba Serikali, wamiliki wa makampuni binafsi na viwanda wazingatie uboreshaji wa mishahara na maslahi kwa wafanyakazi ili iendane na kupanda kwa gharama za maisha.
“Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei mosi mwaka huu inatokana na hali halisi ya maisha ya wafanyakazi, kutokana na uwepo wa mishahara midogo na maslahi duni yasiyokidhi hali na gharama za maisha kwa sasa, hivyo tunaomba mishahara iongezwe, ”alisema Mnjema.
Wafanyakazi wakiwa kwenye maandamano kutoka Shirika la Posta kuelekea kwenye viwanja vya CCM Kambarage kuadhimisha siku ya wafanyakazi Meimosi.
Maandamano yakiendelea.
Burudani za mbio za Baiskeli katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei mosi mkoani Shinyanga.
Wafanyakazi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Meimosi mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Meimosi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi cheti cha Pongezi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura kweye maadhimisho hayo ya siku ya wafanyakazi Meimosi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi cheti cha Pongezi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba kweye maadhimisho hayo ya siku ya wafanyakazi Meimosi
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga