- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Wanawake (UN-WOMEN) imetekeleza Mradi wa Kutokomeza Vitendo vya Unyanyasaji na Ukandamizaji kwa Wanawake na Watoto kwenye maeneo ya masoko katika Manispaa ya Shinyanga. Mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wa mwaka 2017/18 - 2021/22.
Kongamano hilo la majadililiano na watu mbalimbali yakiwemo madhehebu ya Dini, watu mashuhuri, wanasiasa, Kamati za Masoko, wamiliki wa Baa na Mahoteli limefanyika leo tarehe 03-07-2019 katika ukumbi wa Kalinjuna uliopo Manispaa ya Shinyanga
Miongoni mwa malengo ya utekelezaji wa mradi, huu ni pamoja na kutoa elimu na kushiriki kikamilifu katika kupinga unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya masoko ambapo wajumbe walitoa maoni mbalimbali
Ikiwa ni hatua ya kupinga ukatili huo.
Aidha Mwenyekiti wa ALAT-Taifa ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo,Mstahiki Meya
GulamHafeez Mukadam alifungua kongamano hilo kwa kuweka mkazo katika suala hilo la unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na Watoto huku akisistiza kuwepo kwa ushirikiano katika jamii na Upendo jambo ambalo litapunguza ukatili na unyanyasaji katika jamii.
Kwa upande mwingine Katibu wa ALAT-Taifa ndg,Elirehema Moses Kaaya alisikitishwa na vitendo hivyo vya ukatili vinavyoendelea katika Mkoa wa Shinyanga na kuwasihi wajumbe kushikamana kwa pamoja ili kufikia lengo la mradi kwa ufanisi.
Mwezeshaji Godwin Mongi wa Bright Jamii Initiative alizungumzia mada mbalimbali kama vile Ubaguzi na Ukatili,Sababu za ukatili wa kijinsia,Namna mbalimbali za ukatili wa kijinsia,Taasisi zinashughulikia masuala ya jinsia na mwisho akasikiliza maoni ya wajumbe waliokuwa wakijibu swali Kwanini ukatili wa kijinsia unaendelea?
Mwezeshaji Mwajina Lipinga,ambae ni mratibu wa mpango kazi wa kuzuia ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na Watoto alizungumzia mada ya maeneo ya utekelezaji wa mpango ambayo serikali imeainisha ktk kuhakikisha utokomezaji dhidi ya ukatili unafanikiwa.
Mwisho wajumbe walitoa mapendekezo mbalimbali kwa kuainisha vyanzo vya rasirimali watu na rasirimali vitu ili kuendeleza mapambano dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa wanawake na Watoto.
YAFUATAYO NI MATUKIO KATIKA PICHA
Padri akifanya maombi kabla ya kuanza kwa kongamano la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya soko.
Mufti akiomba dua ili kongamano liende vizuri chini ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu
Wajumbe katika kongamano la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya soko,Manispaa ya Shinyanga.
Mwezeshaji Godwin Mongi akiwasilisha Mada katika kongamano la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mwezeshaji Mwajina Lipinga akiwasilisha Mada katika kongamano la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mmoja wa wajumbe akichangia hoja
katika kongamano la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga