- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2025, Ndg. Ismail Ali Ussi, ametoa wito kwa wananchi, hususani vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, kuchangamkia fursa ya mikopo isiyo na riba ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi.
Ndg. Ussi ametoa wito huo leo Agosti 07,2025 alipotembelea na kukagua shughuli za kiuchumi zinazotekelezwa na Kikundi cha Vijana cha Fighter kilichopo Kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga, ambacho kimenufaika na mkopo, Kikundi kilichowekeza katika shughuli mbalimbali zikiwemo ufyatuaji wa wa tofali, uchomeleaji, uuzaji wa samani za ndani na uendeshaji wa shughuli za kifedha.
Katika ziara hiyo, Ndg. Ussi ameeleza kuwa mikopo ya asilimia 10 ni sehemu ya juhudi za Serikali za Awamu ya Sita katika kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi na kupambana na umasikini.
“Mikopo hii haina riba, ni fursa adhimu kwa vijana, akinamama na watu wenye ulemavu kuanzisha au kuendeleza miradi yao ya kiuchumi. Serikali ipo kwa ajili ya kuwainua wananchi wake, hivyo tuitumie ipasavyo,” amesema Ndg. Ussi.
Jumla ya milioni 44,000,000/= wamekopesha vijana wa kikundi cha Fighter .
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga