- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Mwaka kitaifa 2025 Ndg. Ismail Ali Ussi ameipongeza Manispaa ya Shinyanga kwa namna inavyoendelea kuboresha miundombinu ya Shule kupitia Mapato ya ndani ya Halmashaurii.
Ndg. Ussi ametoa Pongezi hizi Leo wakati akiweka jiwe la msingi Katika Ujenzi wa Vyumba viwili na Ofisi ya Walimu pamoja na Samani za kufundishia Katika Shule ya Msingi Kambarage, mradi unaotarajiwa kugarimu jumla ya Milioni 52.
“Haya ni maelekezo mahususi ya Dkt. Samia kuwa mapato yote yanayopatikana ni lazima kutenga Fungu kadhaa ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma, Elimu, Afya na huduma za kijamii, nikupongeze kwa dhati Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kwa kuendelea kutii na kuheshimi maelekezo ya Rais Katika kukarabari mazingira ya kufundishia kwa walimu na kujifunza kwa wanafunzi Hawa wa kata ya Kambarage. Amesema Ndg. Ussi
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga