- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru 2025 ndg. Ismail Ali Ussi ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa namna ambavyo inaendelea kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kupanda Miti na matumishi ya nishati safi ya kupikia.
Ndg. Ussi ametoa Pongezi hizi leo Agosti 07, 2025 wakati akikagua nishati safi ya kupikia kutoka kwa kikundi Cha Wanawake na Samia, Kuzindua bidhaa ya Makaa mbadala, kukagua bustani ya Miti dawa pamoja na kukagua shughuli za vijana wanamazingira kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
“Nimpongeze Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Kagunze kwa ubunifu wa kulifanya eneo hili kuwa la utulivu kwa wakazi wa kata hii , sambamba na kuendelea kuhimiza wananchi juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, Sisi wakimbiza Mwenge wa uhuru mwaka 2025 tumeridhishwa na ubunifu huu kwa asilimia 100”. Amesema Ndg. Ussi.
Pamoja na mambo mengi kiongozi wa mwenge kitaifa Ndg. Ussi pamoja na viongozi mbalimbali walipata muda wa kupanda miti ya matunda katika bustani ya Kagunze ( KAGUNZE GARDEN).
Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira na Utumiaji wa Nishati Safi na Salama kwa Wananchi ni mradi uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 6,136,000.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga