- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KIKAO CHA TATHIMINI YA MKATABA WA LISHE CHAFANYIKA SHY DC
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Johari Samizi, leo tarehe 8 Novemba, 2023 ameongoza Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kilichofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Shinyanga.
Mhe. Johari ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, pamoja na mambo mengine amewaagiza Watendaji wa kata kuhakikisha kuwa wanapanda vitalu vya viazi lishe kwa kila kata.
Amesema hayo ili kuhakikisha kuwa Wilaya ya Shinyanga inaondokana kabisa na matatizo yote yatokanayo na ukosefu wa LISHE BORA.
Aidha, Mhe. Samizi amewataka watendaji wa kata kwenda kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira hasa katika kipindi hiki cha mvua pamoja na kuendelea kutoa tahadhari ya mvua za el nino kwa wananchi na kuendelea kuhamasisha wazazi kwenda kuandikisha watoto wa Darasa la kwanza na awali kwa mwaka 2024.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga