- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KATAMBI ATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO ALIYOWAAHAIDI WANANCHI WA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi,amesema ahadi ambazo aliwahidi wananchi wa manispaa kipindi cha uchanguzi 2020 nyingi amezitekeleza
amebahini hayo leo Marchi 13,2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kitangili kwenye Mkutano wa hadhara.
Mhe. Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, amesema kutokana na machungu aliyonayo kwa wananchi wa Shinyanga, amekuwa akitafuta fedha ili kutekeleza Miradi mingi ya Maendeleo,na kwamba ahadi ambazo alikuwa ameahidi nyingi ametekeleza, huku akitoa fedha za jimbo Sh.milioni 61.6 ambazo zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kila Kata.
“Ahadi ambazo niliwahidi wananchi kipindi cha uchanguzi nyingi nimetekeleza na nina Mshukuru Rais Samia kwa kuniunga mkono na leo kero nyingi zimetatuliwa ikiwamo miundombinu ya Barabara ambayo ilikuwa korofi na Madaraja,” amesema Mhe. Katambi.
Kwa upande wake Mhe. Mariamu Nyangaka Diwani wa kata ya Kitangiri ambapo mkutano wa hadhara ulipofanyika amemshukuru Mhe. Rais Samia pamoja na Mhe. Katambi kwa kumuunga Mkono kwa kufanikisha ujenzi wa Miundombinu ya Barabara na Madaraja ambayo yalikuwa kero kubwa za wananchi,huku akiahidi kuendelea kumalizia kero zilizobaki.
Huu ni muendelezo wa ziara za Mhe. Katambi katika jimbo lake zenye lengo la kusikiliza , kupokea na kutatua kero ambapo katika ziara zake ameambatana na Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga