- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAMATI YA SIASA YA WILAYA YA SHINYANGA MJINI YAIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA ILANI YA CCM 2020/2025
Na. Shinyanga Mc
Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Shinyanga Mjini imeipongeza Manispaa ya Shinyanga kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM 2020/2025 ambapo pamoja na pongezi kwa utekelezaji mzuri wa Ilani lakini pia Kamati imeishauri Serikali kuboresha na kuimarisha kivuko cha wananchi kuingia soko jipya la Ibinzamata.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 3 Juni, 2024 na Ndg. Anord Makombe Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini huku akitoa ushauri wa maboresho mbalimbali yafanyike katika miradi na kutaka ikamilike kwa haraka ili wanufaika waanze kuitumia.
Awali Kamati ilikagua utekelezaji wa Ilani katika Ujenzi wa vyumba vya maabara 2 katika shule ya mwangulumbi, Ujenzi wa Shule ya Sekondari Lubaga, Ujenzi wa Stendi ya Lubaga, Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Manispaa, Ukarabati wa Vibanda Soko Kuu pamoja na Ujenzi wa Soko la Ibinzamata, huku akipongeza zaidi ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD) katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ambapo pia aliwasisitiza wahudumu wa afya kuzingatia kwa uadilifu, maadili ya utendaji wa kazi bora na kutoa huduma nzuri kwa wananchi.
“Tuipongeze Serikali kwa utekelezaji wa Ilani yetu ya CCM 2022/2025 katika sekta ambazo Kamati imekagua, na kwamba maelekezo na ushauri uliotolewa na Kamati uzingatiwe na utekelezwe haraka zikiwemo kasoro zote zilizobainika ili wananchi wanufaike na utekelezaji huu wa Ilani”, amesema Ndg. Makombe
Kwa upande wa Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amesema kuwa, Serikali imepokea kwa unyenyekevu na uzito mkubwa maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Siasa ya Wilaya na kwamba ndani ya muda mfupi Serikali itakuwa imetekeleza kikamilivu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga