- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAMATI YA SIASA MKOA WA SHINYANGA YAIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA ILANI YA CCM 2020/2025
Na. Shinyanga Mc
KAMATI ya Siasa Mkoa wa Shinyanga imeipongeza Manispaa ya Shinyanga kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM 2020/2025 ambapo pamoja na pongezi kwa utekelezaji mzuri wa Ilani lakini pia Kamati imeishauri Serikali kuboresha na kuimarisha kivuko cha wananchi kuingia soko jipya la Ibinzamata.
Hayo yamebainishwa tarehe 24 Februari, 2024 na Ndg.John Siagi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga ambaye alimuwakilisha Mwenyekiti CCM Mkoa wa Shinyanga Ndg. Mabala Mlolwa ambaye alipata udhuru huku akisisitiza pia uboreshwaji wa mazingira katika Shule mpya ya Sekondari Butengwa ambapo amewataka kuongeza kupanda miti ya matunda na vivuli.
Awali Kamati ilikagua utekelezaji wa Ilani katika Shule mpya ya Wasichana Shinyanga ambapo ameitaka Serikali kusimamia vema ujenzi wa majengo ili yawanufaishe na vizazi vijavyo, huku akipongeza zaidi ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharula katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ambapo pia aliwasisitiza wahudumu wa afya kuzingatia kwa uadilifu, maadili ya utendaji wa kazi bora ukizingatia kuwa wanahudumia wananchi.
“Tuipongeze Serikali kwa utekelezaji wa Ilani yetu ya CCM 2022/2025 katika sekta ambazo Kamati imekagua, na kwamba maelekezo na ushauri uliotolewa na Kamati uzingatiwe na utekelezwe haraka zikiwemo kasoro zote zilizobainika ili wananchi wanufaike na utekelezaji huu wa Ilani”, amesema Ndg. Siagi
Kwa upande wa Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ambaye hakuwepo baada ya kupata udhuru alisema kuwa, Serikali imepokea kwa unyenyekevu na uzito wa aina yake maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Siasa Mkoa na kwamba ndani ya muda mfupi Serikali itakuwa imetekeleza kikamilivu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga