- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI ( PAC) YATEMBELEA MRADI WA UBORESHAJI USALAMA WA MILIKI ZA ARDHI MANISPAA YA SHINYANGA.
Na Shinyanga Mc.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imetembelea Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Miliki Ardhi za Manispaa ya Shinyanga, na kuwataka wananchi wachangamkie kupata Hati Miliki
Ziara hiyo imefanyika leo Marchi 20, 2024 kwa kuona shughuli ambazo zinafanyika za kutambua,kupanga,kupima na kumilikisha wananchi Ardhi kwa kuwapatia Hati Miliki.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge (PAC) Mhe. Japhet Hasunga, amesema Kamati hiyo kazi yake ni kusimamia na kuona Fedha za Umma ambazo ziliidhinishwa na Bunge, namna zinavyofanya kazi na kuleta tija kwa Wananchi na kuonekana thamani yake.
“Sera ya Bunge tunataka kila kipande cha Ardhi kipimwe na kupangiwa Matumizi ili tuweze kusonga Mbele,”amesema Mhe. Hasunga.
Aidha, amewataka wananchi wasiishie tu kwenye upimaji na utambuzi, bali wahakikishe wawe na Hati Miliki, na kwamba wakiwa na Hati Miliki eneo hilo ndiyo linakuwa la kwao kihalali.
Kwa upande wake Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda, amesema Mradi huo ni Mkakati wa kutatua Migogoro ya Ardhi na Mipaka, pamoja na kuweka vizuri Mipango bora ya Matumizi ya Ardhi.
Aidha Mhe. Pinda amesema kwa migogoro yote ya Ardhi ambayo ilikuwepo hapo awali, Mradi huo ndiyo umekuja kuitatua pamoja na wananchi kupata Hati Miliki ya Maeneo yao.
Naye Afisa Mipango Miji Manispaa ya Shinyanga Ndg. Emmanuel Mitinje, amesema kwa Manispaa ya Shinyanga wameanza kupima katika maeneo ambayo yalikuwa yamejengwa Kiholela ili kupanga Miji pamoja na kurasimisha wananchi wapate Hati Miliki.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga